Wakala wa barabara za vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Ikungi,Mkoani Singida inatarajia kutumia jumla ya shilingi 3,872,547,262.47 kwa ajili ya kukamilisha miradi ya matengenezo ya barabara,miradi ya maendeleo,ujenzi wa madaraja,fedha za usimamizi wa miradi na fedha za kuendeshea shughuli za ofisi.
Meneja wa TARURA Wilaya ya Ikungi,Mhandisi Ally Mimbi aliyasema hayo alipokuwa akitoa taarifa ya mpango wa matengenezo ya barabara na madaraja kwa mwaka wa fedha wa 2025/2026.
Mhandisi Mimbi hata hivyo alifafanua kwamba mpango huo wa bajeti,una jumla ya matengenezo ya barabara yenye urefu wa kilomita 103.1,kalvati sanduku 18,makalvati mistari 27,ujenzi wa mitaro mita 900,ukarabati wa drifti 1,ukarabati wa madaraja 4 na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami mita 700 zitatekelezwa.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa