Ufunguzi wa utambuzi na uandikishaji wa kaya maskini kwa vijiji Arobaini na nne (44) ambavyo havikufikiwa na mapango wa Awamu ya kwanza kuzinduliwa leo Tarehe 25/05/2021. Mheshimiwa Mkuu wa Wiilaya Ndg. Edward Mpogolo wa tatu kutoka kushoto amefungua hafla hiyo na kufurahishwa na Serikali kwa jinsi ambavyo inawajali watanzania wa hali chini. Aidha amesisistiza kuwa watendaji watakaohusika kubaini kaya maskini wafanye kazi kwa weledi bila kuwa na upendeleo wa aina yeyote. Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Ikungi Ndg. Justice Kijazi wa pili kutoka kushoto , ameishukuru Serikali kwa kupatiwa kaya nyingine Arobaini na nne (44) ambazo awali hazikuwepo kwenye mpango. Ndg . Justice Kijazi amesema kuwa Halmashauri ya Willaya ya Ikungi ina vijiji 101 ambavyo kwa sasa vyote vipo kwenye mpango. Awali vijiji 57 vilikuwa kwenye mpango lakini kwa sasa baada ya kuongezeka vijiji 44 vijiji vyote vimefikiwa na mradi
Habari Picha
Mheshimiwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg. Ally Mwanga wa kwanza kutoka kulia, akifuatiwa na Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya Ndg, Edward Mpogolo (katikati) pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa kwanza kutoka kushoto wakijadili jambo kabla ya uzinduzi wa mpango wa TASAF III Awamu ya pili kwa vijiji 44. Mapacha hawa watatu wanaonesha nyuso za furaha kwani wanafanya kazi kwa upendo na ushirikiano mkubwa jambo ambalo limeifanya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kushamiri.
Mkuu wa Wilaya akiongea jambo kwa wawezeshaji watakaofanya zoezi la kubaini kaya maskini katika vijiji 44.
Washiriki wa semina ya uandikishaji wa kaya maskini wakionesha kuwa makini kusikiliza somo ikiwa ni siku ya kwanza ya mafunzo hayo, ambayo yatafanyika kwa muda wa siku tano katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.Aidha Semina hiyo kwa siku ya kwanza ilishirikisha Kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya, Waheshimiwa Madiwani, Wakuu wa Idara na Vitengo na wawezeshaji walioteuliwa kuandikisha kaya maskini,
Mwenyekiti wa Halmashauri akiwaasa washiriki wa mafunzo ya Mpango wa TASAF III Awamu ya pili
Mkurugenzi Mtendaji akizungumza jambo na washiriki wa mafunzo ya Mpango wa TASAF III Awamu ya pili
Afisa ufuatiliaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Nuru Mkomambo akijibu maswali kwa ufasaha yaliyoulizwa na washiriki wa mafunzo ya utambuzi na uandikishaji wa kaya masikini TASAF III Awamu ya pili
Matukio mbali mbali katika picha
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa