Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida ni moja ya Halmashauri zilizoibuka kidedea katika mashindano ya SHIMISEMITA 2022 kati ya Halmashauri 54 zilizoshiriki mashindano hayo yaliyofanyika Mkoa wa Morogoro...
Tarehe 08 Novemba,2022 kwa niaba ya uongozi watimu pamoja na wachezaji wamemshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi kwa kuiwezesha timu ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo na hatimaye kuibuka kidedea katika mashindano hayo ikiwa ni mara yao ya kwanza kushiriki tangu tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo...
Katika mashindano hayo TImu hiyo ilisindikizwa na vionngozi mbalimbali Akiwemo Afsa Utamaduni na Michezo wa wilaya Ndg kennan Jey Kidanka,Afsa Utumishi Julias Method Kafuku pamoja na wachezaji 25 wakiwemo wakiume 16 na wakike 9 Kwa lengo la kushiriki mashindano hayo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa