Afisa Tawala wa Wilaya ya Ikungi Ndg.Jackson G.Kibeba akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Thomas C.Apson pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Rashid M.Rashid ameongoza zoezi la usafi wa mazingira katika mnara wa mwenge uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi katika siku ya mashujaa.
Akisimulia historia ya mashujaa kabla ya kuanza zoezi la usafi mapema hii leo tarehe 25 Julai, 2024 Afisa Tawala amesema kuwa kila ifikapo Julai 25 ya kila mwaka,Tanzania huadhimisha siku ya kuwakumbuka mashujaa waliopoteza maisha yao wakiutetea, kuupigania na kulinda Uhuru wa Tanzania hivyo hii pia huambatana na shughuli mbalimbali ikiwemo dua na sala maalum za kuwaombea Mashujaa waliopoteza masiaha na kuimbea Amani ya Nchi kutoka kwa Viongozi wa Dini.
Afisa Tawala ameongeza nakusema kuwa Mashujaa hao walipambana kwa hali na mali kwa ajili ya kuitetea Nchi ya Tanzania wakiwa katika maeneo mbalimbali walijizatiti na kujitoa kwa uzalendo mkubwa kwa kuweka rehani maisha yao kwa ajili ya Tanzania.
"Hivyo uongozi, menejimenti na wananchi wote wa Wilaya ya Ikungi tunaungana na watanzania wote kuwakumbuka na kuwaombea kheri Mashujaa wetu kutokana na kujali na kudumisha misingi ya amani." Amezungumza Kiongozi huyo
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Haika Massawe amesema kuwa misingi mizuri na imara iliyojengwa na waasisi wa Taifa letu Baba wa Taifa Hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume, imesababisha Wananchi wa Tanzania kwa muda mrefu kuishi kwa Amani na Utulivu huku wakifanya mambo yao kwa uhuru bila kuingiliwa na mtu yoyote wa ndani au nje.
"Hivyo amani iliyojengwa imepelekea wageni, wakimbizi na watalii kuifanya Tanzania kuwa kivutio na kimbilio" amesema Bi Haika.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa