Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Thomas Apson Ahitimisha Mafunzo ya Mradi wa Upishi Safi,Punguza kazi bila malipo kwa mjadala,maswali na majibu kutoka kwa wawezeshaji.Akizungumza kwenye hafla hiyo kabla haja hitimisha mafunzo Tarehe 19 Disemba 2023 katika ukumbi wa Ofisi yake Dc Apson amesema kuwa ni wakati wa kumpunguzia mwanamke shughuli ambazo hazimuingizii kipato ili aweze kusaidia kuingiza kipato kuanzia ngazi ya familia na kuendelea."Mradi huu ni mzuri kwani utamuwezesha mwanamke kuinuka kiuchumi ila msijisahau kuwa mnapaswa kuwaheshimu waume zenu kwani wao ndio vichwa vya familia hata vitabu vya dini vinaandika hivyo pia"Alisema Mhe DcMradi huu unatekelezwa na Mtandao wa Nishati na Jinsia Tanzania TANGSEN kwa ufadhili wa UN Women katika Wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida ambapo ulianza mwezi wa 10 na kuhitimishwa mwezi wa 12 mwaka huu.Mtaalam Mshauri TANGSEN Bi Gisela Ngoo amesema shirika hili linatoa elimu na kuhamasisha matumizi ya Teknolojia zinazorahisisha kazi kama majiko ya kisasa ambayo ni safi na bora."Naishauri Serikali kuweka sheria ndogo ndogo zinazolenga kupunguza mzigo wa kazi zisizo na malipo katika Halmashauri Kata na Vijiji"Amesema Mtaalamu Mshauri wa TANGSENTafiti zinaonyesha wastani wa masaa 3 mpaka 6 hutumiwa na wanawake kutafta kuni kila wiki kwa ajili ya kupikia,na hutumia wastani wa masaa 4 mpaka 6 kupika sawa na wastani wa masaa 35 kwa wiki bila malipo hivyo yakitumika majiko ya kisasa muda huo unapungua mpaka wastani wa masaa 18 kwa wiki na kumsaidia mwanamke kufanya shughuli zingine zenye kumuingizia kipato katika familia.MWISHO Imetolewa na,Afisa HabariHalmashauri ya Wilaya ya Ikungi19/12/2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa