Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Singida imekagua miradi mbalimbali inayotarajiwa kupitiwa na Mwenge wa Uhuru mwaka huu katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.
Ziara hiyo imefanyika hii leo
tarehe 12 Julai, 2025 ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Halima Omary Dendego ambaye amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuupokea Mwenge huo, huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kudumisha usafi wa mazingira na upandaji miti pamoja na kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu ili kuchagua viongozi watakao waletea maendeleo.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na
Shule mpya ya Sekondari Amali Samamba, Mradi wa maji Wibia, Mradi wa vijana uchomeleaji Ikungi, Mradi wa mfumo wa gesi shule ya Sekondari Ikungi, Ujenzi wa Njia za watembea kwa miguu hospitali ya wilaya Ikungi, Mradi wa engo la utawala TFS, ujenzi wa Barabara pamoja na ujenzi wa kiwanja cha michezo.
Hata hivyo RC Dendego amepongeza maandalizi ya mwenge katika wilaya ya ikungi kwani kumekuwa na mapokezi makubwa pamoja na ubora wa miradi kwa kuzingatia maelekezo waliyopewa.
Kaulimbiu ya Mwenge kwa mwaka huu ni: “Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu.”
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa