Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt Fatma Mganga, leo Novemba 3 ,2023 katika kikao cha M-MAMA amesema kuwa Wakurugenzi kila mwezi wajitathimini kwa kiasi gani wamechangia kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa kupitia mfumo wa M-MAMA .Pia wasimamie vituo na kuchukua hatua kwa watumishi wasio wajibika .Dkt Mganga amesisitiza Waganga wa kuu kutoa elimu kila mara kwa jamii kwa kutumia televisheni wawapo vituoni na waongeze utoaji wa huduma zote kwa wakati na kuwajali wagonjwa ili M-MAMA iendane na vitu vyote.Ameongeza kwa kusema kuwa mfumo wa M-MAMA lengo kubwa ni kuongeza uharaka wa huduma utakao saidia mama na mtoto kufika kituo cha afya mapema kwaajili ya kupata huduma na kupunguza gharama kwa jamii.Mwisho Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Singida ,Iramba,Ikungi,Singida ,Manispa na mkalama wamepokea maagizo hayo na kuahidi kuyatekeleza lengo kufika asilimia 70 ya upungufu wa vifo vya mama na mtoto Mkoani Singida.imeletwa kwenu na kitengo cha habari na mawasiliani serikalini.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa