Kikao cha kawaida cha kamati ya kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto MTAKUWWA cha wilaya ya Ikungi chajadili taarifa za utekelezaji wa miradi kutoka divisheni ya Maendeleo ya jamii katika huduma ya afya ,ustawi wa jamii na lishe.
Akisoma taarifa ya mpango wa Taifa wa kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto MTAKUWWA katika ripoti ya mwaka Juli 2024-Septemba 2024 Bi-Robby Muhochi Afisa Ustawi wa jamii amesema kuwa kumekuwa na changamoto jamii kutokutoa ushirikiano kuhusiana na wahanga wa ukatili, jamii kutoshiriki kikamilifu katika mikutano inayotoa elimu juu ya ukatili wa kijinsia.
Katika kikao hicho wajumbe wametoa maoni juu ya taarifa hiyo kuwa elimu iendelewe kutokewa kwa jamii, kubaini na kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi, huduma ya mkono kwa mkonoONE STOP CENTER kuchukua mkondo wake inapobidi.
Aidha mikakati imewekwa ili kuendelea kudhibiti matukio ya ukatili wilaya ya Ikungi kama vile kamati mbalimbali za MTAKUWWA kukaa na kujadili namna ya kutokomeza janga hilo, kuhamasisha wananchi kutoa taarifa za ukatili, kuhamasisha wananchi kushiriki mikutano ya elimu dhidi ya ukatili.
"Hata hivyo tunashirikiana kwa karibu na kitengo cha lishe kutoa elimu ya uhifadhi wa chakula kwa jamii ili kuepuka ukosefu wa chakula katika kaya na kuhatarisha ulinzi na usalama wa afya ya mama na mtoto" amezungumza Afisa Ustawi
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi-Haika Massawe ambaye pia ni mwenyekiti wa kikao hicho wakati akifunga kikao amesema kuwa kuna haja ya wazazi kupewa elimu hasa kipindi hiki cha likizo watoto wanapokua nyumbani kwani ndiko yanakotokea matukio ya ukatili zaidi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa