Katibu Tawala Wilaya ya Ikungi Mhe. Rashid M. Rashid atoa wito kwa wadau na jamii kwa ujumla ndani na nje ya Wilaya ya Ikungi kuungana na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwakumbuka wenye uhitaji wakati hasa katika kipindi hiki cha sikukuu za krismasi na mwaka mpya.Hayo yamesemwa leo tarehe 29 Disemba 2024 katika hafla fupi shule ya msingi Dung'unyi kituo cha watoto wenye uhitaji maalimu takribani 24 ambapo Katibu Tawala amesema kuwa zaidi ya zawadi zenye thamani ya laki 7 na elfu arobaini na nne zimetolewa katika kituo hicho."Nipende kuwapongeza na kuwashukuru walimu na walezi pamoja na wadau wengine ndani ya Wilaya ya Ikungi kwa jitihada zao katika kuyahudumia makundi yenye uhitaji, Juhudi hizo zinadhihirisha wazi kuwa Wadau na jamii kwa ujumla wanavyo unga mkono zuhudi za Serikali kuhakiksha kuwa Makundi maalumu au wenye uhitaji wanapata huduma stahiki" amesema Mhe Rashid.Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Andrew Marwa amezichukua changamoto alizobainisha Mkuu cha kitengo watoto hao na kuahidi kuzitatua kubwa ikiwa ni pamoja na uhaba wa walimu na vitendea kazi katika kituo hicho cha watoto wenye mahitaji maalumu.Kituo hicho kilianza rasmi mnamo mwezi januari mwaka 2024 kikiwa na chini ya usimamizi wa mwalimu wa elimu maalumu Jilu Muna Mpanda kikiwa na watoto 7 kati yao wavulana wakiwa ni 6 na wasichana ni 1, haladi sasa kituo kinasimamiwa na mwalimu wa elimu maalumu Elibariki Mundogo Clement ambapo kina wanafunzi 24 kati yao wavulana 12 na wasichana ni 12.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa