Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Mheshimiwa Thomas Apson, amefanya kikao kazi na maafisa tarafa pamoja na watendaji wa kata na vijiji leo, Septemba 19, 2025, katika ukumbi wa Halmashauri.
Katika kikao hicho, Mheshimiwa Apson amesisitiza mambo kadhaa muhimu ikiwemo ubunifu katika kukuza mapato ya halmashauri, kusikiliza kero za wananchi ili kuhakikisha wanapata huduma bora, kutatua migogoro mbalimbali inayojitokeza, na kusimamia miradi ya maendeleo na kuwataka kutoa taarifa za mara kwa mara katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Aidha, amewasisitiza kufanya vikao vya kijiji ili kuwaelimisha wananchi kujitokeza kukopa mikopo ya asilimia 10 inayotokana na mapato ya ndani kwani ni mikopo itakayowakwamua kiuchumi na isiyo na masharti magumu.
Vilevile, Mheshimiwa Apson amewasisitiza kutekeleza majukumu yao kwa bidii na kujitoa kwa moyo wa kizalendo kwa kuwa wameaminiwa, hivyo wanapaswa kuwahudumia wananchi kwa uadilifu na uwajibikaji.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa