Afisa Tawala wa Wilaya ya Ikungi Mhe Jackson Kibeba tarehe 30 julai 2024, amemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ikungi kwenye kikao cha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kufikia 30 juni 2024.
Mhe Jackson Kibeba katika kikao hicho amewashauri wakala wa usambazaji wa maji na usafi wa mazingira vijiji (RUWASA) kushirikiana vizuri na muwekezaji mkubwa wa kijiji cha choda(ALFRADAWS investment Company Limited) kwani ana mitambo mikubwa inayoweza kuchimba kwenda chini zaidi.
Katika kikao hicho Kaimu Meneja Eng Michael Ndunguru amesema lengo la serikali katika kipindi cha mwaka 2020-2025 ni kuona kuwa nchi inaendelea kuwa na usalama wa maji na kwamba huduma ya majisafi na salama inaendelea kuimarishwa na kuwafikia zaidi ya asilimia 85 ya wakazi wa Vijiji na zaidi ya asilimia 95 kwa mjini ifikapo mwaka 2025.
Pia wahasibu wa CBWSO wa kata zote za Wilaya ya Ikungi wamewasilisha taarifa za mafanikio kwa kila kata za huduma za maji na changamoto zinazowakabili kwa watumia maji pamoja na wao.
CDO Mkoa wa Singida amesisistiza wasimamizi wa maji kuwa na mahusiano kati ya wateja wa maji na vyombo ili kujua changamoto zao ,wawe na vikao vya mara kwa mara,kuwavutia wateja kwa kutoa huduma bora,kutoa taarifa sahihi kwa wateja na kutoa huduma ya maji kwa usawa.
Mhe Dule wa kata ya Makiungu amesema Makiungu kuwe na tanki kubwa kwani uhitaji wa maji ni mkubwa na kushauri wawe wanafanya ukaguzi wa mabomba mara kwa mara kwani kuna wizi wa mita na ukataji wa mabomba .
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa