Maadhimisho ya Kilele cha wiki ya maji kufanyika katika kijij cha Ntewa Wilayani Ikungi
Posted on: March 22nd, 2018
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Singida Mwandisi. Jackson Masaka akiwa na Viongozi mbali mbali kutoka Singida Manispaa,Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Manyoni, Itigi, na wananchi wa kata ya Kituntu Wilayani Ikungi wameadhimisha Kilele cha wiki ya maji Kimkoa yaliyofanyika kijiji cha Ntewa Kata ya Kituntu Wilaya ya Ikungi. Kauli Mbiu“HIFADHIMAJI NA MFUMO WA KIIKOLOJIA KWA MAENDELEO YA JAMII”.
Shughuliizi za Maadhimisho ya Kilele cha wiki ya maji zimeanza kwa uzinduzi wa Kioski cha maji katika eneo la Bima kilichojengwa na mamlaka ya maji na maji taka Singida mjini. Kioski hiki kimezinduliwa na Katibu Tawala wa Mkoa waSingida Dkt. Angelina M. Lutambi.
Maadhimisho ya kilele cha wiki ya Maji hufanyika Tarehe 22/03 kila mwaka Nchini Tanzania.Aidha Asilimia ya 44.3 ya wakazi waishio vijijini katika Mkoawa Singida wanapata huduma ya maji safi na salama. Idadi ya Vituo vya kuchoteamaji. Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ina idadi ya vituo 766, SingidaManispaa ina Idadi ya vituo 251,Halmashauri ya Wilaya ya Iramba ina idadi yavituo 719. Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama ina idadi ya vituo 468,Halmashauriya Wilaya ya Singida inavituo 716, Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni ina vituo 492, Halmashauriya Wilaya ya Itigi ina idadi ya vituo 127 na Kaimu mkuu wa Mkoa amewapongeza waandisi wote wa Halmashauri za Wilaya zote za Mkoa wa Singida kwa kutekeleza Miradi mbali mbali ya Maji Mkoani Singida. Pia amewashukuru wananchi kwa ushirikiano wa kuadhimisha kilele cha wiki ya maji Wilayani Ikungi Mkoa waSingida.
VileVile Amewashauri kuacha kukata miti ili kuwa na mazingira bora. Amewaasa wananchi wa Kata ya kituntu kutupa shoka na kukamata mzinga kwa ajili ya kufuga nyuki ili kutunza mazingira, Kupata mvua ya kutosha pia kuhifadhi mfumo wa maji kwa maendeleo ya jamii.