Abushiri Juma amekuwa mtoto wakwanza kupata chanjo ya Surua na Rubella katika kituo cha Afya Ikungi aliyopatiwa na Muuguzi Lena Daudi katika uzinduzi wa chanjo hiyo uliofanywa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Radhid M.Rashid akiongozana na Ndg.Justice Kijazi Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wakimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Thomas Apson.Akizungumza kabla ya kuzindua zoezi la chanjo hiyo katibu tawala amesema kuwa wilaya ya Ikungi ina jumla ya walengwa elf 55 ambao watapatiwa chanjo hiyo kuanzia leo tarehe 15 hadi tarehe 18 mwezi huu.Ameongeza na kusema jumla ya timu 80 zitafika katika maeneo yote Wilaya ya Ikungi kwaajili ya zoezi hili na kila timu itakuwa na mchanjaji, mtakwimu, na mhamasishaji ambaye jukumu lake ni kuhamasisha jamii kushiriki kupatiwa huduma hii"Nitumie fursa hii kuwaalika wananchi wenye watoto wenye umri wa Kuanzia miezi 9 hadi 59 kupata huduma ya chanjo kituo chochote Kilichopo karibu yake"amesema katibu tawala.Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi ametoa pongezi kwa wadau wote walioshiriki, kuitikia wito na kuonyesha utayari katika utekelezaji wa kampeni hii ya kitaifa katika Wilaya yetu ya Ikungi kukabiliana na magonjwa ya Surua na Rubella hasa kwa watoto wadogo"Tuondoe dhana zinazojengwa na watu wengine kuwa chanjo hizi zina madhara kwa watoto, Mama yetu Samia Suluhu anatupenda na amethibitisha kuwa hii chanjo ni muhimu kwa watoto wetu tuitumie kuwakinga thidi ya magonjwa haya ya mlipuko"amesema Mkurugenzi.Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Dkt Dorisila ameleza kwamba zoezi hili limefadhiliwa na mfuko wa pamoja wa chanjo na kinga GAVI ambapo fedha zilizotengwa jumla ni Milioni 63.2 ya bajeti ya fedha zilisotengwa na Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi."Chanjo imekwisha sambazwa katika vituo vyote vya kutolea huduma hivyo ameagizi mratibu wa zoezi hilo kuhakikisha zoezi hili la siku tatu linaenda sawa na vifaa tiba vinapatikana muda wote" amezungumza Mganga Mkuu
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa