Balozi wa pamba Tanzania Agrey Mwanri azindua msimu wa kilimo 2022/2023 kwa kampeni ya kuongeza tija na uzalishaji wa pamba...
Semina hiyo imefanyika hii leo tarehe 6 Octoba 2022 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi na kusema kuwa Ikungi ina ardhi ambayo inafaa kwa uzalishaji wa zao la Pamba."Neema na baraka za Ikungi zimefungwa katika zao la Pamba hivyo ukitaka utajiri lima Pamba"Alisema Agrey...
Kwa upande wake Afisa Kilimo Bodi ya Pamba Mkoa wa Singida Abrahaman Athuman amesema msimu ulioisha Mkoa wa Singida haukufikia malengo katika uzalishaji wa Pamba kutokana na hali ya hewa ila awamu hii Mkoa umejiwekea malengo ya kupata kilogramu Milioni 15."Naiomba Bodi ya Pamba ituunge mkono kuifikia adhima yetu" Alisema Afisa Kilimo Mkoa wa Singida...
Semina hiyo ilihudhuriwa na wakulima 151 kutoka kata mbalimbali wilayani hapo ambao kwa nyakato tofauti tofauti walimshukuru Balozi wa pamba kwa Mafunzo wanayotoa na kuahidi kutekeleza waliyofundishwa na Balozi huyo.
Afisa Habari
Halmashauri ya Ikungi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa