Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi Mhe Mika Likapakapa Akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Singinda Mhe Peter Serukamba Awataka viongozi wa Dini kuhubiri Amani,kwa maendeleo endelevu dhidi ya umasikini ujinga na maradhi hasa katika kipindi hiki cha sikuu kuu za Chrismas na Mwaka mpya.
Akizungumza hii leo tarehe 28 Desemba 2022 na Jumuia ya maridhiano mkoa wa Singida Katika kongamano la viongozi wa dini Wilaya ya Ikungi ambalo kwa mara ya kwanza limefanyika mkoa wa Singida wilaya ya Ikungi katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Likapakapa amesema kuwa lengo kuu la jumuiya hiyo ni kuleta amani kwa maendeleo endelevu dhidi ya ujinga na maradhi na umasikini.
"Tumeona na tumeunga mkono Serikali ya awamu ya sita ya Mama Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania."
Kwa upande wake Mbunge wa Ikungi Mashariki Mhe Miraji Mtaturu ameongeza na kusema kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya Amani na Maendeleo hivyo viongozi wadini hawana budi kushirikiana kwa karibu na viongozi wa serikali ili kuleta amani na maendeleo ya Ikungi.
Mhe Ally Juma Mwanga ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Richard Rwehumbiza Wamesema kuwa serikali inatoa fedha nyingi za miradi na watahakikisha usimamizi wa miradi hiyo unakuwa mkubwa ili kutokuvunja amani katika wilaya hii.
Aidha kwa upande wake Mkuu wa polisi wilaya ya Ikungi Bi Suzana A.Kidiku pamoja na Mkuu wa Takukuru Wilaya ya Ikungi Bwn Erick Nyoni wamesisitiza kuepukana na rushwa pamoja na ukatili wa kijinsia kwani ndio adui mkubwa wa Maendeleo.
Pia Ambwene Stephen Makamu Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Singida katika kampeni yao ya kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto na Manawamke amewaomba wananchi kutoa taarifa mapema dhidi ya vitendo vya ukatili ili kuepusha migogoro katika jamii zetu.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa