VIONGOZI WASHIRIKI ZOEZI LA SENSA YA WATU NA MAKAZI.
Na Amour Eljabry Singida
Viongozi mbalimbali wa kitaifa tayari wameshafikiwa na zoezi la sense ya watu na makazi lililoanza rasmi tarehe 23/8/2022 ili kuwa chachu na mfano wa kuigwa kwa wananchi. Baadhi ya viongozi walioripotiwa kufikiwa na zoezi hilo ni pamoja na Rais wa jamhuri ya muungano wa T anzania Mhe. Samia Suluhu Hassani, Mawaziri mbalimbali , wabunge na viongozi mbalimbali wa kimkoa.
Mkoani singida baahdi ya viongozi waliohesabiwa ni pamoja mbunge wa Iramba ambaye pia ni waziri wa Fedha mh. Mwigulu Nchemba, mkuu Wilaya ya Singida Mhandisi Paskazi Mragili, Mkuu Wa mkoa wa singida Mhe. Peter serukamba na viongozi wengineo.
Akiongea baada ya kuhesabiwa nyumbani kwake Utemini Singida mkuu wa mkoa wa Singida alisema
“usiku wa kuamkia tarehe 23 mwezi huu makarani wa sense wa mkoa wa singida walitembelea maeneo mbalimbali ikiwemo vituo vya basi, mahospitali, nanyumba za kulala wa genii li kuanza zoezi la sensa”
Naye mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry C.Muro ameshiriki zoezi la sensa ya watu na makazi kwa kuhesabiwa akiwa katika makazi yake Ikungi mkoani Singida.
Zoezi la kuhesabiwa limeongozwa na karani wa sensa ya watu na makazi Bi. Scovia mkempia deus akiwa pamoja na mwenyekiti wa kitongoji cha gairo kijiji cha Ikungi Bw. Justin Juma Mghwai
Mkuu huyo wa wilaya ametimiza takwa la kisheria la kuhesabiwa ametoaushirikiano kwa kujibu maswali yote 100 ipasavyo na watu wa kaya yake
Muro pia amewapongeza sana waratibu na wasimamizi wa zoezi hilo wakiwemo karani na mwenyekiti kwakuf anya kazi yao kwa uadilif u na umakini mkubwa, wakiwa wakarimu na waungwana katika uulizaji wa maswali
Ametoa rai kwa wananchi wote wa Ikungi kuendelea kuwapokea na kuwapa ushirikiano wa kutosha makarani wetu wa sensa iii waweze kuif anya kazi hii kwa uaminif u na uadilif u mkubwa katika zoezi hili la sensa ya watu na makazi 2022
Picha na matukio
Karani wa sensa ya watu na makazi Bi. Scovia mkempia deus akiwa pamoja na mwenyekiti wa kitongoji cha Gairo kijiji cha Ikungi Bw. Justin Juma Mghwai wakiwachukua taarifa za sensa ya watu na makazi Nyumbani kwa DC Muro
Waziri wa fedha Mhe. Mwigulu NChemba NAYE ametiza zoezi la kuhesabiwa akiwa nyumbani kwake Iramba Singida.
Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe. Peter serukamba akiwa pamoja na karani wa sense baada ya kumaliza kuhesabiwa
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa