• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Ikungi District Council
Ikungi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Elimu msingi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Maji
      • Ujenzi
      • Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • Tekolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Biashara
    • Madini
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Mipango na Utawala
      • Elimu, Afya na Maji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbailmbali
    • Fomu Malimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Vituo vya habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya picha
  • Takwimu za Wilaya
    • Sensa 2022
      • Matokeo ngazi ya Taifa na Mkoa
      • Matokeo ngazi ya wilaya na kata
      • Matokeo ngazi ya vijiji
      • Kasi ya ongezeko la watu
      • Idadi ya kaya
      • Idadi ya watu kwa umri
      • Matokeo ngazi ya tarafa
    • Takwimu za Elimu
      • Orodha ya Shule kwa kata
      • Idadi ya wanafunzi
        • Msingi
        • Sekondari
    • Nyanja ya Afya
      • Idadi ya vituo vya afya kwa kata
      • Afya nyinginezo
    • Ikungi yetu
    • Takwimu za miradi

Wachimbaji Wadogo Watakiwa Kuijua Sheria ya Madini na Kanuni Zake

Posted on: June 22nd, 2025

Naibu waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa amewataka wachimbaji wadogo wa madini kuijua Sheria ya Madini sura namba 123 na Kanuni ili kuondokana na migogoro sehemu za uchimbaji madini ambayo hupelekea kurudisha nyuma maendeleo ya kazi.

Dkt.Kiruswa ameyasema hayo leo Juni 22, 2025 Wilaya ya Ikungi wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uchimbaji na uzalishaji madini katika machimbo mbalimbali yaliyopo kata za Matongo na Mang'onyi mkoani Singida.

Dkt.Kiruswa ameeleza kuwa kutokana na utafiti uliofanyika imeibainika kuwa, moja ya sababu inayoleta migogoro katika maeneo ya uchimbaji ni pamoja na kufanya uchimbaji pamoja na kumiliki leseni ya uchimbaji bila kuijua Sheria ya Madini na Kanuni ambapo amewataka wataalam kutoka Ofisi ya Madini Mkazi Singida kutoa elimu kuhusu Sheria ya Madini na Kanuni zake.

Dkt. Kiruswa ameongeza kuwa, pamoja na Sheria ya Madini pia wachimbaji wadogo wanatakiwa kufahamu kuhusu Mpango wa Uwajibikaji kwa Jamii zinazozunguka mgodi (CSR) na Mpango wa Manunuzi kwa Wazawa (Local Content)   kwa faida ya wamiliki wa leseni  kujua sehemu ya  wajibu wao.

Akielezea kuhusu changamoto zilizopo kwa wachimbaji wadogo wa Kata Matongo, Dkt. Kiruswa ameeleza kuwa, Serikali inatambua changamoto mbalimbali zilizopo akitolea mfano changamoto ya barabara , nishati ya Umeme na maji na kuahidi kuwa katika Mwaka wa Fedha 2025/2026 zitapewa kipaumbele kuzitatua.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Thomas Apson amesema, wilaya ya Ikungi imefanikiwa kupunguza migogoro katika maeneo mbalimbali ya wachimbaji wadogo ambayo ilikuwa inahusisha ardhi , leseni na maduara ya uchimbaji katika Kata zinazoizunguka  wilaya ya Ikungi.

Akibainisha kuhusu mchango wa Sekta ya Madini, Apson ameipongeza Wizara ya Madini kwa juhudi inazofanya katika mageuzi ya mifumo ya kiutendaji na ushirikishaji wa kisekta ambayo inaleta matokeo chanya  kiuchumi.

Awali, akitoa taarifa ya maendeleo ya Sekta ya Madini, Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Singida Mhandisi Sabai Nyansiri amesema , Ofisi ya RMO, Singida inaendelea kuimarisha ushirikiano katika ngazi mbalimbali za mkoa kuanzia Uongozi wa mkoa, wilaya na Taasisi za Umma kwa lengo la kuendelea kuongeza maduhuli ya serikali kutoka Sekta ya Madini.

Kuhusu hali ya migogoro kwa wachimbaji wadogo ngazi ya mkoa na wilaya , Sabai amefafanua kuwa, Ofisi inaendelea na utatuzi wa migogoro ya muda mrefu na muda mfupi inayohusisha wachimbaji wadogo wenyewe kwa wenyewe , migogoro baina ya  wamiliki wa leseni na wamiliki wa ardhi kwa kushirikisha ngazi zote za mkoa ili kutatua kwa haraka bila kuleta madhara kwa jamii.


Matangazo

  • MPYA! MPYA! MPYA! TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI SEPT 06, 2023 August 31, 2023
  • View All

Habari mpya

  • Ziara ya Ukaguzi wa Miradi Siku 10 Kabla ya Mwenge, RC Dendego Apongeza

    July 12, 2025
  • Ripoti ya Utafiti wa Msitu wa Minyughe Yatolewa, Matarajio Mema Ikungi

    July 10, 2025
  • Elimu Itolewe Mfumo wa Stakabadhi Ghalani

    July 09, 2025
  • Kampeni ya Kitaifa ya Chanjo ya Mifugo Yazinduliwa Rasmi

    July 08, 2025
  • View All

Video

DC Muro atembelea Kata ya Mkiwa na kukagua ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari Mkiwa. Kazi inaendelea...
More Videos

Viunganishi vya haraka

Tovuti unganifu

  • EGA website
  • public service management
  • TAMISEMI website
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi

    Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania

    Simu ya mezani: +255262964037/6

    Mobile:

    Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa