Kamati ya huduma za uchumi tarehe 2 agosti 2024 ,ikiongozwa na mwenyekiti wa Halmashauri wa Wilaya ya Ikungi Mhe Ally mwanga wamejadili taarifa za idara mbalimbali ikiwemo idara ya kilimo,mifugo na uvuvi,miundo mbinu,maendeleo ya vijijini na mijini,Idara ya viwanda na biashara na uwekezaji,Idara ya maliasili na hifadhi ya mazingira pamoja na Kitengo cha uthibiti taka na usafi wa mazingira.
Pia waheshimiwa madiwani wamepokea taarifa ya makubaliano ya kufanya biashara ya hewa ya ukaa kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi na Kampuni ya Soldecom Agro Ltd katika hifadhi ya msitu wa Minyughe.
Katika kikao hicho Mhe Shabani Mtakii wa kata ya Makilawa amewataka wataalum kuweka utaratibu mzuri kwa wakala wa mbegu na mbolea ili zifike mapema na kwa wakati na kuisisitiza idara ya miundombinu kuyawekea kipau mbele maboma yote ya muda mrefu katika umaliziaji.
Mhe Herena Uyubu wa kata ya Mungaa amesisitiza swala la ulinzi wa vifaranga vya bwawa la muyanji liwekewe utaratibu mzuri ili vifaranga vya samaki visivunwe kwa kuweka doria ya nguvu.
Mhe Mwandu wa kata ya Ighombwe na Mhe Makomero wa kata ya Mang'onyi wameuliza kwanini wataalamu hawafiki kwenye shule zao kwani ni chakavu sana haswa shule ya Mwau , Sambaru na Mahumbi.
Mwisho mwenyekiti wa kikao Mhe Makangare amehitimisha kwa kusema yote yaliyojadiliwa yafanyiwe kazi haswa kwa wale waanga wa kuathiriwa na Tembo kifuta machozi kiwe kinawahi ,pembejeo zije mapema na kusisitiza kijiji(halmashauri ya kijiji) kusimamia swala la ulinzi wa vifaranga vya samaki .
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa