Katika kikao cha kawaida cha wafanyabiashara Wilaya ya Ikungi cha kujadili maswala mbalimbali ya kibiashara Mkuu wa Wilaya Mhe. Thomas Apson amesema kuwa kuna umuhimu wa kutoa mikopo hasa kwa wajasiriamali ili kukuza biashara zao.
Wakijadili hii leo tarehe 20 Juni, 2025 katika kikao hicho amesisitiza wajasiriamali kupatiwa mikopo ili waweze kukuza mitaji yao.
DC Apson ameongezqa na kuseama kuwa wafanya biashara pia wanapaswa kulipa kodi kwani adhima ya serikali ni kuhakikisha kila mwananchi anainuka kiuchumi
“Hata hivyo Kupitia kodi zenu miradi mbalimbali inaweza kujengwa katika maeneo kadha wa kadha hivyo kulipa kodi ni muhimu" amesisitiza DC Apson
Baraza hilo pia limejadili yatokanayo maazimio ya kikao cha biashara cha tarehe 16 Januari, 2025 juu ya mapendekezo ya kuwekwa kwa mazingira mazuri (shades) kituo cha wafanyabiashara kideka, kubadili aina ya mazao na kupendekeza kilimo cha biashara kama alizeti na mazao mengine ya biashara mashamba ya Issuna, kufanya mkutano wa kimataifa kupitia mitandao ikihusisha TIC na wadau mbalimbali wa biashara pamoja na kuwa na soko la madini katika Wilaya ya Ikungi na maazimio hayo yote yametekelezwa kama ilivyoazimiwa.
Akiwasilisha taarifa kutoka divisheni ya biashara juu ya mfumo wa ukusanyaji wa mapato kwa wafanyabiashara, Afisa Biashara Bi- Mariam Juma Abdallah Wilaya ya Ikungi ameeleza uwepo wa mfumo mpya wa ukusanyaji wa mapato TAUSI katika ngazi ya serikali za mitaa unavyofanya kazi na faida zake kwa wafanyabiashara kuwa inarahisisha ulipaji wa kodi na kupata mikopo kirahisi.
Naye Afisa Biashara Greceana Msofe amesema kuwa serikali imeanzisha mfumo wa vitambulisho vya wajasiriamali wadogo chini ya wizara ya maendeleo ya jamii ikilenga kuwafikia makundi maalumu kama vile Mama ntilie, Babantilie, Boda boda pamoja na bajaji
“Hivyo vitasaidia wafanyabiashara kupata mikopo kwa urahisi na usajili wake unamashariti machache kama kuwa na nambari ya nida, namba ya Simu ambavyo vitatumika kama dhamana.”amefafanua Greceana.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa