Halmashauri ya wilaya ya ikungi wakishilikiana na kampuni ya uchimbaji wa madini Shanta Mining wametoa mafunzo na kuelimisha wajumbe wa kata na vijiji vya unyahati pamoja na Issuna kuhusu sumu itakayo pita kwenye maeneo yao kutoka Daresaalam hapo jana 19 january 2023.
Maneja wa kampuni hiyo ndg Elisante alisema kuwa sumu hiyo aina ya sayanaidi ina uwezo wa kuua binadamu pamoja na wanyama endapo itadondoka eneo fulani wakati wa usafirishaji na kukutana na maji kwa muda mfupi.
Pia ndg Elisante amesema kuwa wananchi wasiogope kwa kuwa sumu hiyo itakuwa imefungwa kwenye vifungashio maalum kwa ajili ya usafirishaji .Pia kutakuwa na magari ya kusindikiza Gari hiyo maalum ili kuangalia usalama wa watu na wanyama endapo sumu hiyo itadondoka kwa bahati mbaya kwa njia ya ajali au namna nyingine.
Katika mafunzo hayo alisisitiza kuwa ni wajibu wao kutoa mafunzo kwa kwa wajumbe wa kata na vijiji walio pembezoni wa barabara itakayopita Sumu hiyo aina ya Sayanaidi kwa ajili ya usalaama wa wananchi hao .
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa