Taasisi ya utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kutoka Kituo cha Naliendele Mkoa wa Mtwara yatoa mafunzo ya nadharia na vitendo juu ya Kilimo cha zao la Korosho na matumizi sahihi na salama ya viuwatilifu katika zao hilo. Mafunzo hayo yamefanyika mapema hii leo tarehe 10 Septemba, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi ambapo Maafisa Kilimo Wilaya na Kata pamoja na wakulima zaidi ya 52 wameshiriki mafunzo hayo. Wakati wa kufungua mafunzo hayo Afisa Kilimo Wilaya ya Ikungi Ndg. Gurisha Msemo ameeleza faida mbalimbali za Kilimo cha zao la Korosho na jinsi zao hilo linavyokuwa kwa kasi kwenye soko la dunia ambapo baadhi ya nchi zinazosafirisha Korosho kwa wingi kutoka Tanzania ni pamoja na India, Pakistan Vietnam na China.Pia Msemo aliendelea kuelezea kuwa zao la Korosho ni zao la muda mrefu hivyo wakulima wa Wilaya ya Ikungi wanatakiwa walime zao hilo na tayari Halmashauri kwa kushirikiana na vijiji vya Mkiwa na Ulyampiti wanetoa mashamba yenye zaidi ya ekari 4,500 kwaajili ya kilimo cha pamoja ( Block Farming ) ya zao la Korosho. Kwa upande wao wawezeshaji wa mafunzo hayo wamesema kuwa Korosho haiitaji udongo wa mfinyanzi haiitaji joto kali wala baridi haiitaji mvua kubwa wala upepo mkali na hali hii ya hewa inapatikana mikoa ya Kanda ya Kati hivyo inawezesha korosho kukua kwa urahisiMuwezeshaji ameongeza na kusema nafasi za upandaji wa miche ya Korosho ni mita 12 kwa 12 kwenye kila upande na shimo lake ni futi mbili kwa mbili na mkulima anapaswa kudhibiti visumbufu kwa njia ya kupogolea na kupanda mazao ya msimu kwa nafasi kwa kuzingatia kanuni za kilimo.Kwa niamba ya wakulima walioshiriki mafunzo hayo Ndugu Ayub Sengo aliishukuru serikali ya awamu ya Sita kwa kutenga bajeti kubwa kabisa katika sekta ya kilimo na kusema kwasasa wameanza kupata ruzuku ya viuatilifu vya zao la Korosho na kumshukuru Mkurugenzi Mtendaji na timu yake ya Idara ya Kilimo kwa huduma ya ugani inayotolewa kuanzia ngazi ya Kijiji,Kata juu ya uzalishaji wa zao la Korosho."kwa sasa nimeanza kuvuna na msimu uliopita amepata tani 2.4 za Korosho jambo linalonipa moyo kuendelea zaidi na naomba mafunzo ya namna hii yatolewe mara kwa mara" amezungumza .
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa