Wakulima Kata ya Mang'onyi wapata mafunzo ya Ushirika pamoja na kuongeza kipato kupitia uzalishaji wa zao la ufuta ambalo litauzwa kwa kupitia mfumo wa stakabadhi mazao Ghalani katika msimu wa 2023/24. Mafunzo hayo yameendelea kutolea kwa Ushirikiano baina ya Mgodi wa Shanta Gold Mine pamoja na Wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Idara ya Kilimo Ikiongozwa na Mkuu wa Idara Ndg Gurisha MsemoMafunzo yamehusisha wakulima viongozi, watendaji wa vijiji vyote, Wenyeviti wa Vijiji, wataalamu wa kampuni ya Shanta Gold Mine,wataalamu wa Kata na Wilaya Lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha wananchi wa Kata ya Mang'onyi kuwa na chanzo kingine cha mapato nje ya kutegemea uchimbaji wa Madini pekee au kilimo cha mazao mengine.Afisa Kilimo Bwana Gurisha Msemo amewaomba wananchi watakaopata elimu hiyo wajitahidi kujikita katika kilimo cha ufuta ili kukuza kipato chao hii ni kulingana na hali ya hewa pia inayotegemewa katika mwaka wa kilimo unaokuja.MWISHOAfisa HabariHalmashauri ya Wilaya ya Ikungi14/09/2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa