Afisa Kilimo Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ambaye pia ni Mwenyekiti wa SIFACU,Mwakilishi Bodi ya Tumbaku na watu wa Benk NMB Gurisha Msemo amewataka wakulima kufata kanuni za kilimo ili kupata mazao bora na kukuza kipato cha wananchi wanaojishughulisha na kilimo hapa nchini...Akizungumza na vyombo vya habari hii leo Tarehe 22 Machi,2023 Afisa kilimo huyo ameeleza kuwa wakulima ni muda wao mzuri kulima kwa tija na kuondokana na kilimo cha kawaida lengo ni kupata mazao mazuri. "Hili ni Shamba la zao la Tumbaku ambalo linapatikana katika Kijiji cha Kipunda Kata ya Mtunduru Wilaya ya Ikungi,Mwaka 2022 August palifanyika uhamasishaji wa Kilimo cha zao la Tumbaku kwa ukanda huo na Wakulima wapatao 9 waliitikia wito huo na kuweza kulima kwa msimu wa 2022/2023 na haya ndio matokea wa zao hilo la Tumbaku." Alisema Afisa Kilimo Ikungi (Tazama picha za matukio
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa