Waheshimiwa Madiwani wasisitiza Walimu kujengewa nyumba.Katika kikao hicho cha kamati ya huduma za jamii hapo Jana 5 February,2024 waheshimiwa wamesisitiza walimu wajengewe nyumba za kuishi ili wawe karibu na mazingira ya shuleni kwani makazi ya watu maeneo mengi ni mbali kutoka shuleni lengo walimu wafundishe kwa wakati na kwa ufanisi zaidi. Mhe Gabriel Dulle,Abel Nkuwi na Abel Suri wameomba shule za Mve ,Nali na Matongo zifanyiwe ukarabati wa haraka kwani ni shule kongwe zimekuwa chavu mno lengo kuepuka maafa haswa kipindi hiki cha mvua.Pia Mhe Suri ameongeza kwa kusema kitengo cha TASAF kiangalie walengwa wenye sifa kweli wa kupewa pesa hizo na kutoa mafunzo kwa mikataba wanayowapa ili kupata uelewa zaidi.Mhe Leornad Nkwae nae ameomba kwenye bajeti ya 2024/2025 awekewe bajeti walau ya chumba kimoja cha maabara cha shule ya Sekondari Iseke Muungano pamoja na kumaliziwa boma la shule mpya ikhoree lililojengwa na nguvu ya wananchi .Mwisho Mwenyekiti wa kamati hiyo ya huduma za jamii Mhe Stephani Missai amesisitiza watoto waliofikia umri wa kwenda shule waende shule, wanafunzi waendelee kupata lishe mashuleni ili kuongeza ufaulu na wazazi wajitahidi kufuatila maendeleo ya watoto wao mashuleni.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa