Mratibu wa uchaguzi wa serikali za mitaa Bi-Haika Massawe ahamasisha wananchi kujiandaa na zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kujisajili kwenye daftari ifikapo kipindi cha kujiandikisha Tarehe 11 mpaka 20 mwezi Octoba 2024 katika vituo vya kujiandikisha vitakavyokwepo katika kila kitongoji. Hayo yamesemwa Tarehe 27 Agosti, 2024 katika kata ya Dung'unyi alipotembelea na kuzungumza na wananchi kijiji cha Damankia na Samaka ili kuwapa elimu juu ya umuhimu wa uchaguzi wa serikali za mitaa. Bi Haika amesema ana Imani wananchi wa Samaka watajiandikisha na kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa ili kuwapata viongozi watakaoshirikiana kwa karibu na wananchi kuleta maendeleo kwa kasi kubwa. "Nahamasisha pia wanawake na watu wenye ulemavu kugombea nafasi za uongozi kwani Wana haki ya kupiga na kupigiwa kura katika uchaguzi huo" amesema MratibuMariam Mwandikile ni Afisa Maendeleo ya jamii yeye ameeleza sifa za mpiga kura kuwa awe raia wa Tanzania, mkazi wa kitongoji husika, awe amejiandikisha kwenye daftari la mpiga kura, awe ametimizamiaka 18, awe na akili timamu na vingine kadha wakadha. Sambamba na hilo Mwandikile ameeleza sifa za mgombea anapaswa kuwa mtanzania, awe na miaka 21, awe ana akili timamu, awe anajua kusoma na kuandika kiswahili au kingereza, awe kwenye chama chochote cha siasa, awe na shughuli halali za kumuongezea kipato Mwisho wananchi wamefurahishwa na elimu hiyo na wameomba elimu hiyo itolewe mara kwa mara ili wananchi kuwa na uelewa wa kutosha juu ya ushiriki wao katika kuchagua viongozi
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa