Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi Mhe Ally Mwanga awataka wananchi kuepuka ngono zembe ili kuepusha ongezeko la maambukizi ya virus vya ukimwi.
Hayo yamesema leo tarehe 24 octaba 2022katika kikao cha kawaida cha kamati ya kudhibiti ukimwi alipokuwa akizungumza na wanakamati alisema kuwa kuna wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari kuepukana na maambukizi hayo kwa kutumia kinga na kupima virus vya ukimwi mara kwa mara
aidha kamati hiyo imejadili ajenda kadha wa kadha ikiwemo kuwasilisha taarifa za utekelezaji shughuli za kudhibiti ukimwi robo ya kwanza julai _septemba 2022/2023.
kikao hicho kiliuzuliwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi Ndg Haika Massawe,Katibu mwenyekiti na wakuu wa idara wa kamati hiyo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa