Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mheshimiwa Thomas Apson awaomba wananchi kuzingatia utaratibu wa kumiliki ardhi ili kuepukana na migogoro isiyo ya lazima.
Hayo yamesemwa katika kliniki ya kusikiliza na kushughulikia kero za wananchi tarehe 11 Juni, 2025 ambayo inafanyika kila juma tano ofisi ya Mkuu wa Wilaya ikiwa na lengo la kuhakikisha wananchi wanatatuliwa kero zao.
Mkuu wa Wilaya amesema kuwa kumekuwa na wimbi kubwa la wananchi wanaoingia katika migogoro kwa sababu ya ardhi na hii ni kutokana na uwepo wa watu wachache wanaojipatia ardhi kwa njia za udanganyifu na wengine kutokufuata sheria za ardhi na hivyo kujikuta katika migogoro isiyoyalazima.
“Natoa maagizo serikali za vijiji kufuata sheria kwa kushirikiana vyema na wajumbe wa Halmashauri pale inapotokea eneo linataka kuuzwa au kununuliwa ili kutengeneza muhutasari wa vikao vya mauziano hayo na sio kuwaachia wenyeviti wa vitongoji kuidhinisha mauzo ya ardhi” amesema Mhe. Apson
Kwa upande wake Afisa Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndugu Ambrose Ngonyani amesema kuwa Halmashauri ya kijiji ni mamlaka ya serikali za mitaa yenye wajibu wa kusimamia ardhi yote ya kijiji.
“Hivyo katika kutekeleza wajibu wake, Halmashauri ya kijiji itabidi kuzingatia ushauri, mamlaka, uwezo, madaraka, haki na wajibu wa taasisi na mamlaka nyingine zilizotambuliwa na sheria kuhusiana na ardhi.” Amefafanua Afisa Ardhi
Ambrose ameongeza na kusema kuwa Halmashauri ya kijiji inafanya kazi kama mdhamini kwa niaba ya wanufaika, hiyo chombo chenye madaraka ya mwisho katika usimamizi wa ardhi ya kijiji ni mkutano mkuu wa kijiji na ugawaji wote wa ardhi ya kijiji lazima uthibitishwe na mkutano mkuu wa kijiji.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa