Wanaume washauriwa kuwapenda na kuwahudumia wake zao ili kuepusha migogoro ya familia ambayo imekuwa ikiongezeka kwenye jamii.
Kauli hiyo imesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Thomas Apson katika kongamano la wanawake lililofanyika hii leo tarehe 04 Machi, 2025 katika ukumbi wa Halmshauri kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yanayofanyika kitaifa Mkoa wa Arusha.
Mhe.Apson amesema kuwa mwanamke akiheshimika jamii inakuwa imara kiuchumi, kijamii na hata katika maswala ya uongozi kwani ana haki ya kutoa maoni yake kwa jamii" amesema Mhe.Apson
Kwa upande wake Bi-Haika Massawe akisoma taarifa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Halmshauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg.Kastori Msigala amesema kuwa divisheni ya maendeleo ya jamii kuelekea siku ya wanawake duaniani wametoa usaidizi wa kisheria, elimu ya mikopo ya asilimia 10 pamoja na kushiriki upandaji miti katika shule ya sekondari ya Amali Samamba kata ya Kituntu.
Aidha, kabla ya kongamano hilo Mgeni Rasmi Mhe. Apson ametembelea na kuzindua mradi wa vijana wa IKUWO unaojishughulisha utengenezaji na uuzaji wa mafuta ya kupaka na bidhaa zingine na mara baada ya hapa ametembelea hospitali ya wilaya ya Ikungi jengo la mama na mtoto kutoa zawadi kwa wanaweke na watoto wenye mahitaji maalumu shule ya Msingi Ikungi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa