Timu ya usimamizi na uendeshaji wa huduma za afya mkoa na wilaya imeagizwa kuhakikisha huduma za afya zinawafikia wanajamii wote kwa usawa ikiwa ni pamoja na kushirikisha wanaume kikamilifu ili kuboresha afya zao wenyewe, afya za wanawake, watoto na vijana.
Hayo yamesemwa leo tarehe 12 Disemba, 2024 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kwenye warsha yenye lengo la kuimarisha huduma za afya kwa kushirikisha wanaume katika huduma za afya ya uzazi, mama na watoto.
Bi-Desteria Nanyanga Mwakikishi kutoka Wizara ya Afya akito mafunzo amesema kuwa warsha hii ni muhimu kwani wanaume ndio watoa maamuzi katika familia na hii itasaidia kuvunja vikwazo vya kitamaduni, kuboresha huduma za afya ya uzazi kwa vijana, kupunguza ukatili wa kijinsia na kuhakikisha kuwa wanawake na watoto wanapata msaada muhimu wakati wa ujauzito, kujifungua, na baada ya kujifungua.
Kwa upande wake kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Singida Bi Teda David Sinde akifungua warsha hiyo amesema kuwa matarajio yake mara baada ya warsha hiyo ni kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu ushiriki wa wanaume katika afya ya uzazi, mama na mtoto, kuboresha huduma za afya katika wilaya ya Ikungi na kutumia vyema uzoefu wao kutoa maoni ili mpango huu uweze kufanikiwa.
"Aidha, tunakusudia kuwasilisha na kukusanya maoni na mapendekezo yenu ili kuboresha mwongozo huu na kuhakikisha unafaa kwa utekelezaji ngazi ya mkoa, Halmashauri na jamii kwa ujumla" amezungumza Mganga Mkuu.
Kwa upande wake Bi-Nkinda Shekalagwe mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI akiahiridha warsha hiyo amesema kuwa wote tuliopata elimu hiyo waende kuwa walimu wazuri kwa wenzao ili kuhakikisha huduma za afya wilaya ya Ikungi inakuwa vizuri upande wa afya ya uzazi na lishe.
Baadhi ya wajumbe wakitoka maoni yao katika warsha hiyo wamesema changamoto imekuwa ni umbali na uchache wa vituo vya kutolea huduma za afya, Mila na tamaduni za baadhi ya makabila juu ya mwanamke na mwanaume kuongozana kwenda vituo vya afya ambapo azimio limekiwa ni kutoa elimu kwa jamii kufuta dhana mbalimbali potofu zilizopo ili kuboresha huduma za afya.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa