Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Thomas Apson amewaomba wananchi kutambua na kuthamini mchango wa wanawake ili kuleta usawa katika jamii.Hayo amesema leo Tarehe 30 Octoba 2023 katika hotuba yake lengo ikiwa ni kuhamasisha jamii kutambua na kuthamini mchango wa kazi za huduma na matunzo zinazofanywa na wanawake katika jamii.Tunapojikita katika kuchunguza maendeleo ya jamii yetu hatuwezi kusahau mchango muhimu unaotolewa na wanawake. Wanawake wetu, mama zetu, dada zetu, na binti zetu, wanachangia kwa kiwango kikubwa katika kazi za kila siku zinazowezesha uhai wa jamii yetu”.Amezungumza DC Thomas ApsonNaye kwa upande wake Afisa maendeleo ya jamii Bi Haika Massawe akisoma taarifa mbele ya mgeni rasmi amesema kuwa Halmashauri ya Ikungi kupitia mashirikiano na UN Women wanawake wasiopungua 1000 walinufaika kupitia ushiriki wenye tija kwenye mnyororo wa thamani wa kilimo cha alizeti na mazao ya mbogamboga‘Aidha kupitia miradi mashirikiano hayo hayo wanajamii katika vijiji vinne vya Kipumbuiko, Manang’ana, Irisya na Munyu walinufaika na mpango wa matumizi bora ya ardhi ambapo wanaume, wanawake na vijana wasiopungua 5000 walipokea hati miliki za ardhi (Certificate of Customary Right of Occupancy). Yote haya yalifanyika kati ya mwaka 2021 hadi 2023.Amesema Afisa MaendeleoMiradi hii pia imehamasisha jamii zetu kwa kuungana na mila rafiki na kupingana na mila potovu zinazogandamiza wanawake na watoto wa kike za kutowapatia nafasi kushiriki vema katika kuchangia maendeleo na ustawi wa jamii zetu.MWISHO Afisa HabariHalmashauri ya Wilaya ya Ikungi30/10/2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa