Meneja wa Program kutoka KIWOHEDE amewasilisha taarifa ya utekelezaji akianisha shughuli zilizotekelezwa ambazo ni kuanzisha klabu mbili katika vijiji vya Irisya na Munyu ,kujenga kituo Jumuisho (OSC)ikungi ,kufanya Mkutano wa Mwezi kujadili masuala ya kushughulikia matukio ya Ukatilii wa wa kijinsia na kutoa mafunzo ya stadi za maisha ,ujasiliamali na uongozi kwa wasichana %) watakao jiunga na klabu za wasichana na kuwapeleka katika chuo cha ufundi Mwakata kahama Shinyanga .
Aidha amewasilisha taarifa ya kazi zilizopangwa kufanywa katika kipindi cha Julai hadi septemba 2022 ambazo ni kukamilisha ujenzi wa kituo jumuishi ikungi na kujenga kituo
jumuishi (One stop centre)katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida
Nae mratibu wa Taasisi ya TAHA,amewasilisha taarifa ya shughuli zilizotekelezwa ,ambazo ni kutoa mafunzo ya kilimo bora cha uzalishaji wa mbogamboga na maembe kwa wakulima 179(ke 158 na Me 21).
Pia Halmashauri idara ya kilimo ,ardhi na maendeleo ya jamii wamewasilisha taarifa ya shughuli zilizofanyika ,ambazo ni kuimarisha vikundi vya wanawake na wasichana kwa kuvijengea uwezo wa namna bora ya uendeshaji wa vikundi hivyo na kuongeza uzalishaji wa bidhaa ambapo mkopo wa Tsh 3,000,000.00 umetolewa kwa vikundi,kutoa elimu ya jinsia kwa jamii.
Pia ameelezea kuwa zoezi la ugawaji wa pikipiki zilizotoka TAHA kwa Maafisa Ugani limefanyika na kuandaa hati miliki za kimila zipatazo 6100.
Pia amewasilisha changamoto zilizo kabili utekelezaji ambazo ni upungufu wa rasilimali fedha ili kuwezesha vinara wa jinsia (Gender champions)kufika maeneo /vitongoji vilivyo mbali kwa ajili ya kuhamasisha usawa wa kijinsia .
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa