Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg. Kastori Msigala awataka wafanya biashara kufata taratibu pindi wanapoanzisha biashara zao ili kuepuka usumbufu usiowalazima.
Akifanya ukaguzi wa leseni na Service Levy kwa kushirikiana na wakuu wa Idara na vitengo pamoja na kamati ya mapato leo tarehe 24 Septemba, 2025 maeneo ya biashara mbalimbali Makiungu, amebaini upotevu wa mapato kutokana na baadhi ya wafanya biashara kukwepa ulipaji kodi.
Mkurugenzi amesema kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kufungwa kwa biashara zao endapo watakiuka taratibu zinazowekwa kisheria na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa upande wake Afisa Biashara Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi-Happiness Edward amesisitiza kuwa kila mfanyabiashara apate elimu juu ya umuhimu wa leseni ya biashara inayotolewa kupitia mfumo wa TAUSI PORTAL na viambatanisho vinavyotakiwa ni pamoja na namba ya NIDA, TIN namba, mkataba wa pango au hati ya kiwanja na Tax Clearance.
“Elimu hii tutaendelea kuitoa kwenye Kata mbalimbali ili mfanyabiashara anapotaka kufanya kazi afanye bila usumbufu kwani leseni ni kitu muhimu kwenye biashara yeyote” amezungumza Afisa Biashara.
Ziara hiyo pia imepita kukagua miradi mbalimbali ya ujenzi ikiwa nipamoja na Shule mpya ya sekondari Kinku, Shule ya msingi shikizi Muve, ujenzi wa vyoo Stendi ya Makiungu pamoja na ujenzi wa kituo cha afya katika kijiji cha Minyinga, ambapo baadhi ya miradi ipo hatua za ukamilishaji na mingine katika hatua za awali.
DED Msigala ameagiza miradi ambayo ipo hatua za awali ianze haraka na ikamilike kwa wakati na ambayo ipo katika hatua za ukamilishaji izingatie ubora kutokana na maelekezo ya serikali.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa