Maazimisho ya siku ya lishe Kitaifa pamoja na uzinduzi wa kampeni ya lishe kwa vijana wenye umri wa miaka 9 mpaka 19 Wilayani Ikungi yamefanyika Tarehe 30 Octoba ,2023 katika shule ya Sekondari Unyahati.Katika maazimisho hayo Maafisa Lishe Wilaya ya Ikungi Ndg Nevu Dickson pamoja na Chausiku Ramadhani wametoa elimu ya makundi matano ya chakula kundi la kwanza ikiwa ni Nafaka,Mizizi,na Ndizi mbichi kundi la pili ni vyakula vyenye asili ya wanyama na jamii ya kunde,kundi la tatu ni Mboga mboga, kundi la nne matunda,kundi la tano ni vyakula vyenye asili ya Mafuta,Asali na Sukari. Maafisa lishe wamesisitiza kuzingatia ulaji unaufaa na kuamasisha uanzishwaji wa klabu za lishe mashuleni na ufanyaji wa mazoezi ya kila siku ili kuboresha afya zao.Aidha viongozi hao kutoka Halmashauri pia wamehamasisha utoaji wa chakula kwa wanafunzi wote ili kuhakikisha watoto wanapata walau mlo mmoja kwa siku kuboresha hali zao za lishe.Katika maadhimisho na uzinduzi huo pia Maafisa lishe wamefanya tathmini ya hali ya lishe kwa walimu na wanafunzi kwa kuwapima uzito na urefu ili kujua hali zao za lishe.Mwisho amewataka wananchi wote kuwa utamaduni wa kusoma majarida mbalimbali yanayohamasisha lishe,kusikiliza vipindi vya redio na TV na kuhudhuria mikutano ya lishe na zoezi hili ni endelevu katika Wilaya ya Ikungi. MWISHOImetolewa na;Afisa HabariHalmashauri ya Wilaya ya Ikungi30/10/2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa