Mkuu wa wilaya ya ikungi Mhe. Jerry C. Muro amezindua zoezi la chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa hatari wa kupooza (POLIO) linalolenga kutoa chanjo kwa watoto 97, 575 katika wilaya ya Ikungi
Mhe. Muro amesema hayo wakati akizindua zoezi la chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa hatari wa polio katika ngazi ya wilaya kwenye kituo cha afya ikungi ambapo amesema wamejipanga kuhakikisha vijiji vyote 101 vinafikiwa katika zoezi hilo ambalo amewataka watumishi kuhakikisha wanatoa chanjo kwa kuzingatia idadi ya watoto wote waliopo kwenye wilaya wanafikiwa kikamilifu
Awali Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ikungi Mhe. Ali Juma Mwanga amesema Halmashauri tayari imeshahakikisha vifaa vyote na watumishi wote wanaotakiwa kuwemo kwenye zoezi hilo wanafika katika maeneo yao na tayari vifaa na watumishi wote wa zoezi wameshafika katika vituo hivyo
Kwa upande wake mganga mkuu wa wilaya Dr. Solomon Michael amesema zoezi litaendeshwa kwa kuzingatia kanuni na miongozo yote iliyotolewa na kuwaomba wazazi kuhakikisha wanashirikiana na timu za ufuatiliaji katika kutoa taarifa zitakazowawezesha kuwafikia watoto wote katika maeneo ya vijiji na vitongoji vyote na kusisitiza viongozi wa vijiji kusaidiana na wataalamu kufanikisha zoezi hilo
Tazama picha na matukio
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa