Mkuu wa wilaya Mhe. Jerry Murro amezindua zoezi la chanjo ya polio ya matone tarehe 30 novemba 2022,katika uzinduzi huo Jerry Muro amesema kuwa watoto wote wenye umri wa miezi 0 hadi 59 wanapata chanjo ili kufikia hatua ya kinga ,kutokana na maelezo hayo amesema kuwa tusiangalie asilimia tu bali tuhakikishe tumewafikia watoto wote .”lengo kutokomeza ugonjwa wa ulemavu wa viungo wa ghafla (polio)”.alisema Muro.
Muro ameongeza na kusema kuwa tuhakikishe jamii inakua na uelewa juu ya chanjo ya polio na hasa kwa kutambua madhara yatokanayo na ugonjwa huo.
Katika uzinduzi huo Afisa Afya wa Wilaya Ndg Abiud Abiud amesema kuwa awamu hii tumepokea kiasi cha 101,000 za chanjo ya polio ya matone,na kiwango hiki cha chanjo kinaendana na walengwa waliochanjwa awamu ya tatu ambao ndio walengwa wa awamu ya nne ambao ni 95575.
Pia amesema kuwa Timu 46 zitatoa chanjo kituoni na timu 1756 zitatoa chanjo nyumba kwa nyumba.”chanjo ya polio ya matone itaanza kutolewa kuanzia tarehe 1/12/2022 hadi tarehe 4/12/2022.”Alisema Abiud
Aidha Abiud amesema kuwa kutakuwa na wasimamizi wa hizo timu 54 ambao watasimamia timu hizo 221 na wasimamizi 4 ambao ni wataalam watapita kila tarafa kufanya tathimini ya Watoto ambao hawajapata chanjo,wasimamizi hao watakuwa wanaingiza taarifa za uchanjaji za kila siku kwenye mfumo kupitia simu janja na kutuma moja kwa moja wizarani kupitia mfumo wa ODK collect.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndg Richard Rwehumbiza amesisitiza kuwa viongozi wa dini na wazee maarufu wahamasishe zoezi hili la chanjo ya polio kikamilifu “ ili tufanikiwe hilo,uwajibikaji,ushirikiano na kijituma kati yetu kwa cheo na uwezo na tuliojaaliwa iwe ni chachu ya mafanikio ya zoezi hili lililoko mbele yetu.”Alizungumza Mkurugenzi.
Awali Mwenyekiti wa Halmashauri wa Wilaya ya Ikungi Mhe Ally J. Mwanga,Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Winfrida Funto pamoja na Makamu Mwenyekiti Stehphano Mtyana walisisitiza viongozi kushiriki kikamilifu kuhamasisha zoezi hili.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa