Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Rasilimali Watu, Bi. Edina Palla, ameongoza semina fupi kuhusu maadili kwa watumishi wa umma, yenye lengo la kuimarisha ufanisi na nidhamu katika utendaji kazi.
Akihitimisha semina hiyo, Bi. Palla alisema: “Kila mmoja wenu anapaswa kujiuliza, nimefanya nini tangu nilipoingia asubuhi hadi ninapoondoka jioni?” – akisisitiza dhima ya uwajibikaji binafsi kazini.
Pia alisisitiza kuwa kila mtumishi anapaswa kuwajibika kwa nafasi yake na kuepuka visingizio visivyo vya msingi ili kukwepa majukumu. “Haikubaliki kabisa,” aliongeza.
Akizungumzia mahusiano kazini, Bi. Palla alieleza kuwa kuna umuhimu wa kuwa na mahusiano mazuri miongoni mwa watumishi, kwani uhasama kazini hupunguza ufanisi. Alisema: “Watumishi wa ofisi moja wanapaswa kuelewana, kujaliana na kushirikiana. Mahusiano mabaya yamesababisha baadhi ya watumishi kufikishana TAKUKURU, jambo ambalo ni baya sana.”
Alimaliza kwa kusema tembea yetu,Fanya yetu, matendo na maneno yetu tunapaswa kuwa waangalifu.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa