WAZIRI AWESO AYASAKA MAJI KWA HELKOPTA WILAYA YA IKUNGI-SINGIDA.
Waziri wa Maji Mhe.Juma Aweso ameipongeza Kampuni ya AL FRADAWS Investment Company Limited kutoka Jordan inayofanya uwekezaji katika kilimo Wilayani Ikungi Mkoa wa Singida kuleta suluhisho la upatikanaji wa maji kwa njia rahisi zaidi.
Katika ziara yake hii leo tarehe 27 Julai, 2024 katika mashamba hayo ya uzalishaji wa mbegu mbalimbali kijiji cha Choda wilayani Ikungi amesema amefurahishwa na kampuni hiyo kwa kuja na Suluhisho katika upatikanaji maji kupitia teknolojia ya Pivot Irrigation System.
Waziri wa Maji Mhe.Juma Aweso amesema Teknolojia ambayo inatumiwa na Wizara ya Maji kwa sasa haina uwezo mkubwa wakujua ni wapi maji yanapatika, umbali au kina Cha maji na ubora wa maji hayo kwa afya ya mwanadamu ukilinganisha na Kampuni hiyo ambayo inauwezo wakufanya yote haya kabla ya kuchimba ndani na yupo tayari kuwapa ushirikiano kuhakikisha Wilaya ya Ikungi na maeneo mengine Mkoa wa Singida na Tanzania kwa ujumla wanapata maji yakutosha kupitia teknolojia hiyo.
Kwa upande wake mwekezaji huyo amesema kuwa zaidi ya Bilioni 81 za kitanzania zimetumika kuwekeza katika eneo hilo na changamoto kubwa imekuwa ni maji hivyo endapo Wizara itasaidia kutatua changamoto hiyo uzalishaji utakuwa mkubwa zaidi.
"Tumejipanga kuzalisha mbegu za mazao mbalimbali na kulima mazao kama mahindi alizeti, viazi , vitungu pamoja na soya na tutaendelea zaidi kadri muda utakavyokwenda." amezungumza Muwekezaji huyo
Katika ziara hiyo Mhe Waziri ameambatana na viongozi mbalimbali wa Wilaya ikiwa ni pamoja na Kamati ya ulizi na usalama Wilaya Ikungi, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi pamoja na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi wamepongeza ujio wa kampuni hiyo kwani inaenda kuleta natokeo chanya katika sekta ya ajira kilimo na ajira nchini
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa