Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Devid Silinde amezindua program ya Usamabazaji wa Mbegu za Ruzuku za Alizeti vijijini Msimu wa Kilimo mwaka 2023/2024 katika Mkoa wa Singida huku akiwataka wananchi kutumia ruzuku hii kama fursa kukuza sekta ya Kilimo na hatimaye kuleta pato la taifa.Hayo yamesemwa leo Tarehe 03 Januari 2024 katika Ukumbi wa RC Mkoa wa Singida na kusema kuwa Mkoa wa Singida unapokea jumla ya Tani 600 za Alizeti kupitia wakala wa usambazaji wa mbegu ASA zenye thanani ya Bilioni 8.5Naibu Waziri amesema kuwa viongozi wa Wilaya na Halmashauri wanapaswa kutoa ushirikiano wa karibu kwa wasambazaji wa mbegu hizo ili ziwafikie wakulima wengi kwa kipindi kifupi lengo ni kuwai msimu wa kilimo kulingana na mvua za wastani zinazonyesha kipindi hiki."Natoa rai kwa wakulima kutumia mbegu bora na mbole Mkoa wa Singida na wakulima nchini kote ili kukuza sekta ya kilimo."amesema Naibu WaziriKwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Peter Serukamba amesema kuwa Mkoa wa Singida Serikali inatekeleza usambazi wa mbegu bora na kudhibiti visumbufu viharibifu vya Alizeti lengo ni kuhakikisha Mkoa wa Singida unakua namba moja Tanzania kwa Kilimo cha Alizeti.Pia amesisitizi kuongeza maeneo ya kilimo na kuhakikisha vijana wote wanakwenda shambani,kuongeza utumiaji wa mboleo katika uzalishaji hasa mbolea za ruzuku kama fursa kwa wakulima,Mfumo wa stakabadhi ghalani ili kuongeza faida kwa wakulima kupata bei bora."Halmashauri zitapata mapato mengi zaidi kupitia mfumo huu.Amezungumza Mkuu wa MkoaKwa upande wao Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Thomas Apson,Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Dkt Anton Mwangolombe pamoja na Afisa Kilimo Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Gurisha Msemo wamesema wamepokea mbegu na wapo tayari kushirikiana kwa karibu kuhakikisha mbegu hizo zinawafikia wakulima wote Wilaya ya Ikungi kwa wakati.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa