Baadhi ya wananchi Kijiji cha Mkiwa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida waiomba serikali kuwawezesha vijana wa kijiji hicho kupata mafunzo maalumu ya jinsi ya kukabiliana na tembo waharibifu katika maeneo yao.
Hayo yamesemwa hii leo tarehe 28 Octoba, 2024 katika mkutano wa Waziri wa Maliasiri na Utalii Balozi Mhe Dkt Pindi Chana na wananchi wa eneo hilo ambapo amefika katika Kijiji hicho mara baada ya kuwa na matukio ya uharibifu wa mazao na makazi katika baadhi ya maeneo ya Kijiji chicho ambayo pia ni shoroba (Jia) za tembo.
Aidha Waziri wa Maliasiri na Utalii Balozi Mhe Dkt Pindi Chana ametoa maelekezo ya serikali kwa lengo la kutatua janga hilo moja ikiwa ni kuzitambua korido za tembo kwa kushirikiana na wananchi, kuongeza askari wanyama pori 18 na kutoa elimu kwa wananchi ili kukabiliana na tembo hao, kuongeza vifaa maalumu vya Kudhibiti na kuswaga tembo kuelekea maeneo ya hifadhi, kuwa na Mipango ya matumizi bora ya ardhi ili kutatua changamoto kwa wananchi wa eneo hilo.
Pia amepongeza juhudi za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kwa kuona vyema kuwa na wizara ya Maliasiri na Utalii katika nchi yetu kwa lengo la kuhakikisha wanyama pori wanakuwa sehemu salama bila kuathiri miundombinu pamoja na mazao ya wananchi.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Thomas Apson ameipongeza wizara hiyo kwa kuona vyema kuja kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Mkiwa ili kutatua tatizo hilo ambalo wananchi wamekuwa wakihitaji usaidizi wa karibu kutoka wizara hiyo ya Maliasiri na Utalii.
Kamishna msaidizi mwandamizi wa uhifadhi kanda ya kati, Ndg. Herman Nyanda, akisoma taarifa mbele ya waziri wa Maliasiri na Utalii amesema kuwa jumla ya askari 19 Mkoa wa Singida ikiwa ni askari wanne wilayani Ikungi wamepatiwa mafunzo ya kukabiliana na wanyama pori waharibifu.
"Hata hivyo serikali kupitia TAWA mnamo tarehe 15 Octoba 24 imetoa mafunzo kwa askari Jeshi la akiba Mgambo 94 wilayani hapa kwa lengo la kukabiliana na janga hilo" amezungumza kamishina huyo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa