Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Apson tarehe 29 julai 2024 amesisitiza wananchi wa wilaya ya Ikungi kuchangia maoni kuhusu Dira ya taifa ya maendeleo 2050 kwaajili ya maendeleo ya serikali na kumsaidia Raisi Samia Suluhu Hassan kufanya mambo makubwa Ikungi.Mratibu wa zoezi hilo la ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu dira ya taifa ndg Sitta Maha Elias amesema Dira ni muongozo wakutuonyesha nini cha kufanya kwa mahali gani,kwa jinsi gani, kwa wakati gani na kwa watu gani.Hivyo ,ni muhimu tukashiriki kikamilifu katika kutoa maoni yetu pamoja na kuhamasisha makundi mbalimbali ya wadau kutoa maoni yao kuhusu Dira 2050 .Pia katika kikao hicho wachangiaji wamesema upande wa uchumi kuna mafanikio makubwa ,wameipongeza serikali kwa kufanya mambo makubwa kama kujenga mashule,vituo vya afya ,barabara pamoja na madaraja.Wananchi wa wilaya ya Ikungi wameongeza kwa kusema maeneo ya kuboresha haswa barabara ya Iyumba ,Sepuka na kila kata kuunganishwa kwa kiwango cha lami miundo mbinu ya mkongo wa taifa,ofisi za watendaji kata,kijiji na kitongoji mwenyekiti wa kijiji wawe na ofisi ,nyumba za watumishi,ajira kwa vijana ,tehama ianzie shule za msingi,uwanja wa ndege ,mwaka wa kiislamu utambuliwe,kila mwananchi awe na kipato cha kati,stakabadhi ghalani kuondoa mtu kati,hosteli kwa watoto wa kike mashuleni ziongezeke,madini yawekewe utaratibu wa kutosha ili wananchi wote wanufaike,wakulima kupata masoko na kuhakikisha maadili ya kitanzania hayapotei. Mwisho Mratibu amesema kuna njia ya kutoa maoni kwa kupiga *152*00#,namba 8 .Elimu na namba 4.Dira 2050..
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa