Wananchi wa Wilaya ya Ikungi wapongeza juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan akishirikiana na uongozi wa wilaya kwa kuwezesha ujenzi wa miradi ya huduma za Afya kama Vituo vya afya na zahanati karibu kila kijiji lengo ikiwa ni kutatua changamoto za wananchi kutembea umbali mrefu kutafta huduma wilayani Ikungi.Wananchi wameongeza na kusema kuwa hali ya kuwepo kwa zahanati vijijini itasaidia kupunguza changamoto mbalimbali za kinamama wajawazito na watoto waliokuwa wakipata adha kutokana na umbali wa huduma za afya.Hayo yamesemwa leo Tarehe 26 Octoba 2023 Katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Peter Serukamba alipotembelea Zahanati mpya ya Kijiji cha Mlandala na kuweka jiwe la msingi Zahanati mpya ya kijiji cha Songandogo kabla ya kupata wasaa wa kuzungumza na wananchi na kusikiliza kero zao."Ipo haja ya kumpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi kwa kutoa fedha kupitia mapato ya ndani ili kukamilisha maboma hayo mawili ambayo yalianzishwa kwa nguvu za wananchi na natoa maagizi zahanati hizi zianze kutumika mara moja ifikapo juma tatu ya Tarehe 30"Amesema Mkuu wa mkoa.Akisoma taarifa mbele ya Mkuu wa Mkoa Kaimu Mganga mkuu wa Wilaya Ndg Kikoti amesema gharama za kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya Songandogo ni milioni 50 kutoka serikali kuu,Milioni 15 kutoka Mapato ya ndani ya Halmashauri ambapo Boma lilijengwa na nguvu za wananchi Pia Serikali kuu imetoa milioni 50 kumalizia boma la zahanati ya Mlandala lililojengwa kwa nguvu za wananchi na milioni 14 ni kutoka Mapato ya ndani ya Halmashauri.Naye kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Ikungu Mhe Rashid M.Rashid akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya Ikungi Mhe.Thomas Apson amemalizia na kusema kuwa katika msimu huu wa kilimo serikali imejipanga kuleta mbolea na mbegu za ruzuku na itahakikisha kila kata wanapata kwa wakati ili kuanza kilimo chenye tija kukuza sekta ya kilimo Ikungi.MWISHOImetolewa na:Afisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi26/10/2023WILAYA YA IKUNGI YANG'ARA KWA UJENZI WA ZAHANATI VIJIJINIWananchi wa Wilaya ya Ikungi wapongeza juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan akishirikiana na uongozi wa wilaya kwa kuwezesha ujenzi wa miradi ya huduma za Afya kama Vituo vya afya na zahanati karibu kila kijiji lengo ikiwa ni kutatua changamoto za wananchi kutembea umbali mrefu kutafta huduma wilayani Ikungi.Wananchi wameongeza na kusema kuwa hali ya kuwepo kwa zahanati vijijini itasaidia kupunguza changamoto mbalimbali za kinamama wajawazito na watoto waliokuwa wakipata adha kutokana na umbali wa huduma za afya.Hayo yamesemwa leo Tarehe 26 Octoba 2023 Katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Peter Serukamba alipotembelea Zahanati mpya ya Kijiji cha Mlandala na kuweka jiwe la msingi Zahanati mpya ya kijiji cha Songandogo kabla ya kupata wasaa wa kuzungumza na wananchi na kusikiliza kero zao."Ipo haja ya kumpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi kwa kutoa fedha kupitia mapato ya ndani ili kukamilisha maboma hayo mawili ambayo yalianzishwa kwa nguvu za wananchi na natoa maagizi zahanati hizi zianze kutumika mara moja ifikapo juma tatu ya Tarehe 30"Amesema Mkuu wa mkoa.Akisoma taarifa mbele ya Mkuu wa Mkoa Kaimu Mganga mkuu wa Wilaya Ndg Kikoti amesema gharama za kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya Songandogo ni milioni 50 kutoka serikali kuu,Milioni 15 kutoka Mapato ya ndani ya Halmashauri ambapo Boma lilijengwa na nguvu za wananchi Pia Serikali kuu imetoa milioni 50 kumalizia boma la zahanati ya Mlandala lililojengwa kwa nguvu za wananchi na milioni 14 ni kutoka Mapato ya ndani ya Halmashauri.Naye kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Ikungu Mhe Rashid M.Rashid akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya Ikungi Mhe.Thomas Apson amemalizia na kusema kuwa katika msimu huu wa kilimo serikali imejipanga kuleta mbolea na mbegu za ruzuku na itahakikisha kila kata wanapata kwa wakati ili kuanza kilimo chenye tija kukuza sekta ya kilimo Ikungi.MWISHOImetolewa na:Afisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi26/10/2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa