Zaidi ya Hati 700 zagawiwa katika hafla ya ugawaji wa hati miliki za kimila kwa wananchi wa Ikungi mkoa wa Singida kupitia mradi wa pamoja wa kuongeza kasi ya uwezeshaji wanawake kiuchumi JP-RWEE na asilimia 40 za hati hizo ni hati za wanawake na wasichana.Hayo yamefanyika hii leo tarehe 10 Januari, 2025 katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi ambapo Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mhe. Deogratius Ndejembi amesema kuwa mradi huo ni matokeo ya mradi wa awali ambapo utekelezaji wake unafanyika kuanzia mwaka 2023 hadi ifikapo mwaka 2027 ukitekelezwa na Halmashauri ya wilaya ya Ikungi na wadau kama vile FAO, WFP, UN WOMEN, IFALD na upo chini ya ufadhili wa Sweden na Norway. Mhe. Thomas Apson anasema kuwa changamoto kubwa inayowakabili wananchi wa wilaya ya Ikungi ni uelewa mdogo wa sheria ya ardhi hivyo kupelekea ongezeko la migogoro ya ardhi wilayani hapa.“Ugawaji wa hati miliki za kimila unaofanyika hii leo ni suluhisho la migogoro hio pia tunaishukuru sana wizara kwa kuweka miundombinu rafiki kutokana na mipango ya ardhi” amesema Apson.Akisoma taarifa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi ametaja vijiji 12 vinavyonufaika na mradi huo ikiwa ni pamoja na Kipumbwiko, Wibia, Puma, Samaka, Matongo na vingine.Baadhi ya wananchi wanaonufaika na mradi huo wameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mradi huo ambao ni mkombozi kwao.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa