Kuelekea maadhimisho ya miaka 63 ya uhuru wa Tanganyika wilaya ya Ikungi imeendesha zoezi la upandaji miti katika maeneo mbalimbali.
Hafla ya upandaji miti kiwilaya imefanyika katika chuo cha mafunzo ya ufundi stadi VETA Ikungi mnamo tarehe 08 Desemba, 2024 na imeongezwa na Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe.Thomas Apson.Jumla ya miche ya miti 1000 ikiwemo ya matunda, kivuli, na mbao imepandwa katika eneo la chuo hicho na maeneo mengine ya watu binafsi.
Aidha wananchi mbalimbali walijitokeza kushiriki katika zoezi hilo na kupatiwa miche kwa ajili ya kupanda katika maeneo yao.
Kwa upande wake Afisa Maliasili Hifadhi ya mazingira Bwana Philbert Benedict ametoa wito kwa wananchi kupanda miti katika maeneo yao na kuitunza kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi yanayotokana na uharibifu wa mazingira.
"Zoezi hili la upandaji miti katika wilaya ya Ikungi linaendelea ambapo lengo ni kupanda jumla ya miche ya miti 1,500,0000 katika maeneo mbalimbali" amezungumza Bwana Philbert
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa