Mkuu wa Mkoa Singida Mhe. Peter Serukamba akamilisha ziara yake kwa kuwaomba wasimamizi wa miradi kuongeza mafundi ili miradi hiyo iishe kwa wakati.Mhe Serukamba amesema hayo katika ziara yake ya siku ya pili Tarehe 06 Juni 2023 ambapo ametembelea Shule ya Msingi Matare Mradi wa Boost kata ya Unyahati,Hospitali ya Wilaya ya Ikungi,Ujenzi wa shule ya Msingi Mpya Ikungi B mradi wa Boost,Barabara kiwango cha lami zaidi ya kilomita 1,Kikundi cha vijana cha Kufyatua tofali CCM, pamoja na Shule ya msingi Dung'unyi ujenzi wa madarasa mawili na matundu ya vyoo mradi wa Boost.Mkuu wa mkoa amesema kuwa na mafundi wengi kunasaidia kurahisisha umaliziaji wa miradi kwa wakati na ufanisi zaidi.Ameongeza na kusema kuwa mafundi wanaomaliza miradi kwa wakati na kwa uhakika wapewe kipaumbele lengo ni kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati.Kwa upande wao mkuu wa Wilaya Ikungi Mhe Thomas Apson pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi wameahudi kukamisha miradi iyo kama maagizo ya Mkuu wa mkoa alivyosema katika ziara yake.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa