Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi aanza ziara ya mwezi mmoja kusikiliza kero za watumishi na wananchi katika Wilaya ya Ikungi na kuzitatua pale inapowezekana Katika ziara hiyo ambayo imeanzia Tarafa ya Ikungi Tarehe 16 Februari 2024 katika ukumbi wa Sekondari ya Ikungi kusikiliza kero za watumishi na baadae Kitio cha zamani Cha kupakia abiria kusikiliza kero za wananchi.Baadhi ya kero zilizowasiliswa na watumishi ni pamoja na kuchelewa Kwa mafao ya watumishi pamoja na kulipwa pesa za uhamisho ampapo Bi Margaret Kapolesya Afisa Elimu msingi na awali amejibu maswali hayo kwa kusema Milioni 30 hutoka kila baada ya kipindi kifupi hivyo hutolewa Kwa ngao kwani wanaodai ni wengi na ameahidi kuwa fedha zote zitalipwa kwa awamu hivyo hawanabudi kuwa wavumilivu.Kwa upande wake Afisa Utumishi Bi Edna Pala ameongeza na kusema kuwa malipo hayo yafanyike Kwa wale wenye vigezo pekee kwani Kuna waliohama Kwa hiari na waliohamishwa na waliohama na familia zao lazima waweza kuambatanisha vyeti vya ndoa pamoja na vya watoto wao pia.Kwa upande wa mkutano wa nje kero nyingi zililenga katika migogoro ya Ardhi ambapo Ndg Ambrose Ngonyani Afisa Ardhi Wilaya ya Ikungi alijibu maswali yao na mengine kuyachukua Kwa ajili ya kuyataftia ufumbuzi,kero zingine zilihusu usumbufu wa wanyama pori kama tembo na nyani katika baadhi ya maeneo ambapo Afisa Misitu Bwana Filbert amesema wapo katika mchakato wa kupokea fedha za fidia kutoka wizara husika kwa waliopata madhara na kuzipeleka kwa wahanga wakishirikiana na Bwana Lory Afisa wanyama pori Wilaya ya Ikungi.Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi amesema ziara hii inalenga kuibua matatizo yanayowakabili wananchi ili waweze kuwasaidia pale inapowezekana kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza"Ziara hii ni endelevu na tutapita Tarafa zote nne za Wilaya ya Ikungi ndani ya mwezi huu wapili ili kuhakikisha tunawafikia wananchi wengi zaidi na tunashiriana kwa karibu na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ili kutatua kero hizo" amezungumza Mkurugenzi Kijazi#ziara
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa