Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Peter Serukamba amewataka wananchi kuongeza maeneo ya kulima ili kuwa na uhakika wa mazao ya kutosha kwa ajili ya chakula na biashara.Hayo ameyasema leo Tarehe 16 Novemba 2023 katika ziara yake ya siku moja ya kutembelea vijiji 16 katika Wilaya ya Ikungi kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo,kuzungumza na wananchi na kusikiliza kero zao.Mkuu wa Mkoa amesema kuwa ipo haja kuongeza maeneo ya kulima kwani Serikali kupitia Viongozi wa Halmashauri imelipia mbegu na mbolea ya ruzuku kwa ajili ya wakulima ambayo itawafikia pale walipo kwa bei nafuu."Nakuagiza Afisa kilimo kuanzia Jumamosi ya Tarehe 18 mwezi huu kuleta mbolea kata ya Mgungira na kata zote jirani na hapa ili wananchi wanunue mbolea na Mbegu hiyo kwani kuna uhitaji."Amesema Mkuu wa Mkoa.Aidha katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa amepongeza Juhudi za Wilaya na Halmashauri kushirikiana katika kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kutumia Mapato ya ndani ya Halmashauri hasa Sekta ya Afya, ili kuepusha vifo na maradhi mbalimbali yasiyo yalazima."Mwankalaja wameomba Zahanati Kaimu Mkurugenzi lichukue hilo naamini mtaweza kulifikiria ili kuondoa adha kwa wananchi hawa"Amesema Mkuu wa MkoaAkijibu Moja ya swali ambalo liliulizwa katika vijiji vingi Mratibu Miradi ya REA Wilaya ya Ikungi Lucy Darabe amesema kuwa Wakala wa Nishati ya Umeme Vijijini (REA) unatekeleza mradi katika vijiji 57 Wilaya ya Ikungi sawa na Km 454.21 za msongo wa kati na Km 162.43 za msongo mdogo,ambapo vijiji 41 vimewashiwa Umeme na wananchi wanaendelea kutumia nishati ya Umeme wateja wapya wanaendelea kuunganishiwa Umeme kufikia Tarehe 30 ya mwezi Desemba 2023 vijiji vyote vilivyosalia vitakua vimewaka umeme kama maagizo ya Mkuu wa Mkoa yalivyo.Baadhi ya Miradi iliyotembelewa katika Ziara ya Mkuu wa Mkoa ni pamoja na Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Iyumbu,Ujenzi wa Vyoo,Mradi wa Maji Iyumbu,Ujenzi wa Kituo cha Polisi Magungumka,Kuzungumza na Wavuvi waliopata majanga ya Moto kambi ya Ufana,kutembelea zahanati na kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua papo hapo na zingine kuzibeba kwa ajili ya utekelezaji MWISHOImetolewa na;Afisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi16/11/202Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Peter Serukamba amewataka wananchi kuongeza maeneo ya kulima ili kuwa na uhakika wa mazao ya kutosha kwa ajili ya chakula na biashara.Hayo ameyasema leo Tarehe 16 Novemba 2023 katika ziara yake ya siku moja ya kutembelea vijiji 16 katika Wilaya ya Ikungi kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo,kuzungumza na wananchi na kusikiliza kero zao.Mkuu wa Mkoa amesema kuwa ipo haja kuongeza maeneo ya kulima kwani Serikali kupitia Viongozi wa Halmashauri imelipia mbegu na mbolea ya ruzuku kwa ajili ya wakulima ambayo itawafikia pale walipo kwa bei nafuu."Nakuagiza Afisa kilimo kuanzia Jumamosi ya Tarehe 18 mwezi huu kuleta mbolea kata ya Mgungira na kata zote jirani na hapa ili wananchi wanunue mbolea na Mbegu hiyo kwani kuna uhitaji."Amesema Mkuu wa Mkoa.Aidha katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa amepongeza Juhudi za Wilaya na Halmashauri kushirikiana katika kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kutumia Mapato ya ndani ya Halmashauri hasa Sekta ya Afya, ili kuepusha vifo na maradhi mbalimbali yasiyo yalazima."Mwankalaja wameomba Zahanati Kaimu Mkurugenzi lichukue hilo naamini mtaweza kulifikiria ili kuondoa adha kwa wananchi hawa"Amesema Mkuu wa MkoaAkijibu Moja ya swali ambalo liliulizwa katika vijiji vingi Mratibu Miradi ya REA Wilaya ya Ikungi Lucy Darabe amesema kuwa Wakala wa Nishati ya Umeme Vijijini (REA) unatekeleza mradi katika vijiji 57 Wilaya ya Ikungi sawa na Km 454.21 za msongo wa kati na Km 162.43 za msongo mdogo,ambapo vijiji 41 vimewashiwa Umeme na wananchi wanaendelea kutumia nishati ya Umeme wateja wapya wanaendelea kuunganishiwa Umeme kufikia Tarehe 30 ya mwezi Desemba 2023 vijiji vyote vilivyosalia vitakua vimewaka umeme kama maagizo ya Mkuu wa Mkoa yalivyo.Baadhi ya Miradi iliyotembelewa katika Ziara ya Mkuu wa Mkoa ni pamoja na Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Iyumbu,Ujenzi wa Vyoo,Mradi wa Maji Iyumbu,Ujenzi wa Kituo cha Polisi Magungumka,Kuzungumza na Wavuvi waliopata majanga ya Moto kambi ya Ufana,kutembelea zahanati na kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua papo hapo na zingine kuzibeba kwa ajili ya utekelezaji MWISHOImetolewa na;Afisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi16/11/202
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa