Baadhi ya wananchi wa Tarafa ya Sepuka Wilaya ya Ikungi mkoani Singida walalamika juu ya ucheleweshaji wa fedha za TASAF kwani wananchi wenye hali ngumu kimaisha wamekuwa wakitambuliwa na kufanya kazi kwa mujibu wa taratibu za TASAF kama vile kuchonga barabara, kuchimba mabwawa na shughuli zingine ili waweze kulipwa fedha hizo lakini imekuwa tofauti na matarajio yao.Hayo yamesemwa hii leo tarehe 15 Machi 2024 katika mwendelezo wa ziara ya Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi mtendaji pamoja na wakuu wa idara na vitengo katika kila Tarafa zilizopo wilayani Ikungi ambapo wananchi hao wamelalamika na kusema wamechimba bwawa kwa muda lakini wakati wa malipo ya TASAF hawatambuliki na wengine kutokulipwa kwa kipindi kirefu hali inayopelekea wananchi kuwa na sintofahamu juu ya tatizo hilo.Mratibu wa Mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Kaweso ametolea ufafanuzi wa jambo hilo kuwa taarifa za waliofanya kazi kwa siku 20 kati ya Siku 60 mwaka huu katika Tarafa ya Sepuka zilipokelewa Halmashauri ya Ikungi na kujazwa kwenye mfumo na baadae kutumwa makao makuu kwa ajili ya malipo mapya pale dirisha la malipo hayo litakapo funguka hivyo ni vyema kuwa watulivu mpaka pale malipo hayo yatakapofunguka kwani hayawezi kuchukua mda mrefu kuanzia sasa."Sambamba na hilo TASAF inafanya malipo kulingana na juhudi za kaya kuhudhuria na kufanya kazi katika miradi ya nguvu kazi iliyoibuliwa na vijiji kwa mujibu wa utaratibu" amefanua Mratibu huyoMkutano huo wa kusikiliza kero za wananchi ulihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Thomas Apson ambapo kero iliyozungumzwa zaidi ni pamoja na migogoro ya Ardhi ambapo amemuagiza Afisa Ardhi Halmashauri ya Ikungi Bwana Ambrose Ngonyani kutengeneza mpango wa upimaji wa maeneo ya Tarafa ya Sepuka ili wamiliki kuwa na hati za umiliki wa Ardhi zao kuepusha migogoro inayoendelea.Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi katika kikao cha ndani mara baada ya kusikiliza kero za watumishi amewaomba watumishi wanaodai stahiki zao mbalimbali kuwa wavumilivu kwani tayari pesa zao zimeingia kwenye akaunti za Elimu Msingi na Sekondari tayari kwa kuanza kufanya malipo
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa