Afisa Kilimo Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Gurisha Msemo akishirikiana na viongozi wengine waendelea na zoezi la uhamsishaji wa msimu wa Kilimo katika kata ya Sepuka.Akizungumza na wananchi wa kata ya Sepuka mnamo Tarehe 02 Novemba 2023 Gurisha amesema kuwa Wananchi wote wafate kanuni Bora za Kilimo na kufuata maelekezo ya Mamlaka ya hali ya hewa ili kuepukana na uharibifu wa mazao yao."Kwa mujibu wa mamlaka ya hali ya hewa wamesema kuwa msimu huu wa kilimo unaonesha kuwa mvua zitawahi na zitakuwa ni za wastani na juu ya wastani hivyo ni vyema kuwasikiliza wataalamu na kufata kanuni bora za kilimo."amezungumza Afisa KilimoZoezi la uhamasishaji limeanza tangu kufunguliwa kwa msimu wa kilimo Wilayani Ikungi ambapo linalenga kuzifikia kata zote na mpaka sasa zimefikiwa kata 7.Ndg Gurisha msemo pia tumewahimiza wakulima kuachana na Kilimo cha mazoea na kulima Kilimo cha Mkataba."lengo la hamasa hii ni kuongeza uzalishaji katika Wilaya yetu ya Ikungi lakini pia kufikia tija kwa mazao ambayo wakulima wanazalisha wilayani hapa."Amesema Afisa Kilimo.MWISHOIMETOLEWA NA:AFISA HABARIHALMASHAURI YA WILAYA YA IKUNGI02/11/2023Afisa Kilimo Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Gurisha Msemo akishirikiana na viongozi wengine waendelea na zoezi la uhamsishaji wa msimu wa Kilimo katika kata ya Sepuka.Akizungumza na wananchi wa kata ya Sepuka mnamo Tarehe 02 Novemba 2023 Gurisha amesema kuwa Wananchi wote wafate kanuni Bora za Kilimo na kufuata maelekezo ya Mamlaka ya hali ya hewa ili kuepukana na uharibifu wa mazao yao."Kwa mujibu wa mamlaka ya hali ya hewa wamesema kuwa msimu huu wa kilimo unaonesha kuwa mvua zitawahi na zitakuwa ni za wastani na juu ya wastani hivyo ni vyema kuwasikiliza wataalamu na kufata kanuni bora za kilimo."amezungumza Afisa KilimoZoezi la uhamasishaji limeanza tangu kufunguliwa kwa msimu wa kilimo Wilayani Ikungi ambapo linalenga kuzifikia kata zote na mpaka sasa zimefikiwa kata 7.Ndg Gurisha msemo pia tumewahimiza wakulima kuachana na Kilimo cha mazoea na kulima Kilimo cha Mkataba."lengo la hamasa hii ni kuongeza uzalishaji katika Wilaya yetu ya Ikungi lakini pia kufikia tija kwa mazao ambayo wakulima wanazalisha wilayani hapa."Amesema Afisa Kilimo.MWISHOIMETOLEWA NA:AFISA HABARIHALMASHAURI YA WILAYA YA IKUNGI02/11/2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa