Baada ya kuzinduliwa kwa zoezi la upandaji miti Kimkoa tarehe 07/01/2023 na Mkuu wa Mkoa Mhe Peter Selukamba katika Wilaya ya Ikungi zoezi imeendelea na hadi sasa imesambazwa na kupandwa miti zaidi ya 30,000 kwa kutumia miti iliyooteshwa katika Vitalu viinne vilivyopo Mungaa,Nkuhi(Ikungi).Mitunduru(Sepuka) na Dadu kwa Hisani ya Mfuko wa Miisitu Tanzania (TaFF) ambapo katika kila Kitalu kuna aina ya miti(Species) isiyopungua kumi ikiwepo miti ya mbao kama Gliricia(Gliricia sepum),miti ya kivuli SDA,au miti maji (Trichilia emitica) maembe (Mangifera indica).Zambarau(Syzygium cummnii) na passion(Passiflora edulis)
Pia kuna aina ya miti ya asili na inayohimili ukame kama Mlonge ( Moringa oleifera) na inayosadikiwa kuwa ni dawa na aina nyingine ya mti wa asili unaohimili ukame na pia unafaida kiuchumi ni mgunga gundi (Vachelia drepanolobium) ambao hutoa gundi yenye soko Kitaifa na Kimataifa.
Aidha Idara ya Afya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Imeitikia Wito wa Upandaji Miti na kwa mwaka 2023 imepanga Kuzindua Upandaji Miti leo tarehe 17 January 2023 Katika Hospitali ya Wilaya iliypo Eneo la Unyahati Barabara ya Maghonyi Shanta Mkabala na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa